JINSI YA KUTUMIA COMPUTER YAKO KUPITIA SIMU YAKO
Unajuwa kuna wengi sana wameshindwa ku install window kwenye simu zao kama nlivyofundisha kwenye somo lililopita kama hukuona bofya hapa kusoma
Sasa kushindwa huko bado hatujashindwa maisha bhana mana najuwa kuna watu wengi sana wanatamani kutumia smartphone zao kama compuer... Sasa hii njia nlioleta hapa nadhani ndio itakuwa njia rahisi zaidi ya kukusaidia.
Ok kwa kuanza najuwa bado kuna mtu mmoja anasoma title ya post lakini bado haelewei... Ngoja nijaribu kumwelewesha mtu huyo.
Kwenye title nimemaanisha hivi yani badala ya kukaa pale mezani kwenye ile computer yako na kufanya mambo mbalimbali basi hukai tena pale mezani unaenda kukaa chumbani au nje ya nyumba kabisa huku unaitumia computer iliyoko ndani kwa kutumia smartphone yako... Yani utachokifanya ukiwa nje pale kwenye smartphone yako basi na ndani kwenye ile computer kitafanyika hivyo hivyo... Kama ume play movie kwenye computer yako basi movie ile utaiona pia kwenye simu yako.... ( kuna mtu mmoja bado hajanielewa hapo najuwa😂😂).
Twende Kazi
Zoezi hili haijalishi unatumia aina gani ya mfumo wa simu yani iwe ios au iwe android wote twende kazi njia hii itafanya kazi vema kwenye simu yako na computer yako pia kama utafata hatua kama nitavyo fafanua.
kwenye computer
Kitu cha kwanza unatakiwa uwe unatumia browser ya Google Chrome.... Kama hauna browser ya Google Chrome basi utaweza download kupitia hapo chini na kisha install vema kwenye computer yako...
Download google chrome here.
Baada ya ku download na ku install chrome kwenye computer yako unachotakiwa kufuata kufanya ni kudownload extension ya chrome remote desktop pia nayo utaweza kuishusha kupitia hapo chini...
Download Chrome remote desktop here
Install vizuri extension hiyo kwenye browser yako ya chrome... Baada tu ya installation kukamilika utaona unapelekwa kwenye menu ya google chrome... Bofya kwenye chrome remote desktop kisha utaona unapelekwa kwenye ukurasa ambao unatakiwa uset computer yako .
Nenda mahali pameandikwa My Computer kisha utabofya kwenye mahali pameandikwa Enable Remote Connection baada ya hapo utatakiwa kuinstall ka program kadogo tu cha MB 11 kwenye computer yako na baada ya kumaliza utaona unapelekwa moja kwa moja kwenye ukurasa ambao utatakiwa kuweka password (hapa ni muhimu sana)...weka password yako na usiisahau wala usimwoneshe mtu kisha bofya OK.
Kwenye simu
Moja kwa moja ingia playstore kwa watumiaji wa android au ingia app store kwa watumiaji wa ios kisha utadownload app inaitwa chrome desktop remote download kwa kupitia hapo chini kutokana na aina ya mfumo unaotumia.
Download Chrome desktop remote for android
Download Chrome desktop remote for ios
Baada ya ku install app hiyo kwenye cm yako ifungue kisha utaona inaleta jina la computer yako... Bonyeza jina hilo kisha utaona inakutaka uweke password sasa hapo ndo utaweza zile password za kule mwanzo ulizo create wakati unamalizia setup kwenye computer.... Baada ya kuweka password basi utabonyeza connect hapo hapo utaona kioo cha computer yako kinaonekana kwenye cm yako.
Kama ukimaliza kutumia ili urudishwe kwenye home screen ya simu yako basi utabonyeza neno Stop Sharing hapo utakuwa umemaliza.
Ukishafanikiwa rudisha mrejesho kwa screen shot na wengine waone.
Mwisho
Usisahau ku like page yetu ya facebook ili uwe unapata notification kila tunapotowa post mpya pia pita hapa ku subscribe youtube channel yetu ambapo huko utaweza kuona video za makala mbalimbali yajayo kwa njia ya video. Karibu.
Share na wengine.
Comments
Post a Comment