JINSI YA KU INSTALL WINDOWS KWENYE SIMU ZA ANDROID

Kutokana na ukuaji wa kiteknolojia basi kila siku mambo yanaendelea kuja mapya zaidi na watu wanazidi kuwa watundu zaidi ili kurahisisha  baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuwa magumu labda kwa kukosa jambo fulani.

Basi kwenye post hii tutaangalia ni jinsi gani utaweza kuifanya simu yako kuwa ni window... Hapa utaweza ku install window 10 ×64, window 10 ×86, window 7 pamoja na window XP itategemea ipi ni napendeleo yako lakini sijafanikiwa kuiweka window 8 kwasababu bado haijatengemaa vizuri.

Vitu vya muhimu

> Kitu cha kwanza basi ni lazima ujue uwezo wa simu yako

> simu yako inatakiwa at at least iwe na RAM kuanzia 1GB na kuendelea

> hakikisha tayari una application inaitwa Limbo pc emulator QEMU ARM ×86  inapatikana play store au waweza bonyeza hapa chini kukupeleka moja kwa moja.

Limbo pc Emulator QEMU

Muonekano wa App ya Limbo pc emulator baada ya ku install 

Baada ya kuwa na hivo vitu hapo juu basi utabofya  hapa chini ku download aina ya window inayohitaji.

Window10_×64... ( 2.81GB)

Window10_×86... ( 1.41GB )

Window7... ( 460.5MB )

WindowXP... ( 461MB )


Twende kazi

Baada ya kudownload  file la window unalolitaka Sasa utafata hatua zinazofatia hapa chini, hakikisha unafata hatua hizi kwa makini kabisa ( vitu vyote unafanya kwa kutumia cm yako sio kompyuta )

Hatua

Baada ya yote hayo sasa nenda kwenye File manager kisha tafuta file lilioandikwa Limbo kama lipo acha kwanza.... Rudi kwenye kwenye file la download ambapo utakuta aina ya window ulio downoad.... Baada ya kuikuta window hiyo kumbuka file hilo la window kitakuwa kwenye format ya IMG.... Sasa unatakiwa ku copy file hilo la window kisha nenda kule kwenye file la Limbo alafu paste..... Baada ya kupaste sasa nenda kaifungue App yako ya Limbo kwenye application zako.

baada ya kufungua app ya Limbo

> Kwenye Load machine chagua "NEW" kisha andika jina unalotaka

> kwenye user interface chagua "SDL"

> kwenye archtecture chagua "×86"

> kwenye cpuModel chagua " Qemu32" (muhimu sana)

> kwenye cpu cores chagua moja "1"

> kwenye RAM memory chagua kutokana na uwezo wa ram ya simu yako.... Kama 1GB basi chagua hvyo hvyo.

> kwenye storage chagua hard disk A kwa kuweka "" kisha uchague file lako la window.

> baada hapo scroll mpaka chini kabisa kisha weka "√" kwenye full screen alafu pia weka "√" kwenye landscape kwa chini.

> baada ya hapo rudi tena kwa ku scroll mpaka juu kabisa kisha bofya sehemu Yenye alama ya Play▶

Kuwaka kwa window yako kutategemea na uwezo wa simu yako hvyo kama simu yako haina uwezo kikamilifu basi inaweza kuchukua hata mpaka dakika kumi kuwaka kabisa.

Baada ya kufanya hvyo vyote kwa umakini  Utaona window yako inafunguka vizuri kabisa na hapo kama simu yako inauwezo wa ku connect na screen kubwa basi unaenjoy kama kompyuta ya kawaida tu tofauti itakuwa kwenye graphics tu.

Mwisho

Kumbuka kabla ya kufanya utaona ni kitu kigumu sana alafu vile vile utaona ni process ndefu saana ila wakati wa kufanya utaona ni simple sana.


Bofya hapa kutembelea Facebook page yetu... Usisahau ku Like page yetu ili uwe updated na kila post zitakazotolewa.




Share na wangine Ujanja huu.

Comments

  1. Baccarat - a game where the cards are dealt
    › game-online › 바카라 사이트 추천 game-online Baccarat is the game where the dealer bids two, then the player to the dealer's left, and the player to the right has a hand with the cards in their hand. In this

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts