FAHAMU TOFAUTI KATI NDEGE NA ROKETI

Karibu katika makala hii fupi ambayo inalenga kuwafungua watu ufahamu juu ya tofauti kati ya ndege na roketi.

Kama tunavyohamu kumekuwa na mkanganyiko mkubwa sana juu ya utofautishaji kati ya ndege na roketi kutokana kurisishwa baadhi ya maneno wakati wa ukuaji wetu kisha na sisi kuja kurisisha wadogo zetu maneno ya uwongo juu ya swala hili.

Wengi wetu tumekwisha shuhudia mara nyingi kitu kikipita angani huku kikiwa kinaacha kitu kama moshi au ukungu nyuma yake sasa ngoja nikujuze kile kitu ni nini kisha tutakuja kutofautisha kati ya ndege na roketi.

CONTRAILS

Hili ni neno ambalo linatumika kutambulisha mistari ya mawingu ambayo huachwa na engine za ndege zinapopita angani. Ndege nyingi zinazotumika sasa huweza kupanda juu kwa umbali kilometa 10 mpaka kilometa 15 ambapo katika umbali huwo joto huwa ni dogo sana hivyo Engine za ndege zinapokuwa zinapumua huwaga kuna unyevu unyevu unatolewa ambapo unyevu unyevu huwo hupowa au kuganda na kusababisha kutokea kwa mistari meupe ambayo ukiwa huku duniani chini huonekana kama mawingu. Mara nyingi hali hii ya ndege kuacha mistari ya mawingu nyuma huwaga inatokea kipindi cha baridi. Vile vile Mistari hiyo ya mawingu huwa inaonekana kwa kuhesabika kutokana na idadi ya engine zilizopo kwenye ndege, kama ndege ina engine 4 basi na mistari hiyo itaonekana mi nne na kama ndege ina engine mbili basi na mistari hiyo itaonekana miwili tu.
Picha hii inaonesha ni jinsi gani contrails inavyotokea
Hivyo basi watu wengi sana tumekuwa tukiona ndege hizo zinapita na kuacha mistari hiyo ya mawingu tumekuwa tukiambizana kwamba hiyo ni roketi inapita wakati si kweli kutokana kwamba tumezowea kuona aina ya ndege ndogo ambazo huwa zinapita maeneo ya karibu sana kwa kukadiria kama kilometa moja juu ambapo huwa hakuna baridi kali ukitofautisha na hizo ndege zinazopita kwenye anga za kimataifa katika umbali wa kilometa 10 mpaka kilometa 15 kutoka aridhini.
Muonekano wa contrails ndege inapokuwa umbali mrefu kutoka Ardhini
Tofauti kati ya roketi na ndege.

Roketi

Kwa maana Roketi ni aina kifaa ambacho husafiri masafa ya umbali mrefu ikitiwa nguvu na aina ya engine itambulikayo kama " Rocket Engine" ambapo zimegawanyika katika makundi tofauti kutokana ma matumizi pamoja na nguvu kwa mfano kuna RD-180 ambayo inatumia Mafuta ya Taa yaani mchanganyiko wa kerosene/LOX na nyinginezo nyingi.
Muonekano wa aina mbali mbali za roketi
Kazi za roketi.

Roketi zina matumizi mengi makubwa kutokana na kuwa na nguvu kubwa sana na uwezo wake wa kisafiri umbali wa masafa marefu. Kazi za roketi zinajumuisha..

> usafirishaji wa makombora... Makombora mengi ya masafa marefu mara nyingi huwa yanasafirishwa kwa kutumia roketi pale yanapokwenda kufanya mashambulizi.

> kusafirisha Settelite... Kazi nyingine ya Rocket huwa zinatumiwa kwaajili ya kusafirisha vifaa mbalimbali vya settelite kwenda katika anga za mbali ambapo vifaa hivyo kwa pamoja vikifungwa ndivo tunapata settelite nzima ambazo zipo huko juu angani.

> kusafirisha wachunguzi... Pia kazi nyingine ya rockets huwa zinatumiwa kisafirisha Wanasayansi mbalimbali ambao huenda kwenye anga za juu kwaajili ya uchunguzi wa masuala mbalimbali ya sayansi za anga za mbali.

> kusindikiza vifaa... Kazi nyingine ya rocket huwa ni kusindikiza vifaa  ambavyo huwa ni kwaajili ya kwenda kwenye sayari nyingine au hata kwenye mwezi... Aina hii ya rocket huwa zinasindikiza kifaa hicho mpaka umbali fulani kutoka duniani kisha huishiwa nguvu na kujiachia kisha kudondoka duniani huku zikiacha kifaa hicho kikiendelea na safari.
Rocket ikiwa inaruka kusindikiza space shuttle ( yenye muonekano kama wa ndege)
Sitaongelea upande wa ndege kwasababu kila mtu anajuwa kazi za ndege na kutokana na maelezo hayo hapo juu pamoja picha tayari mtu utakuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya ndege na roketi lakini nataka kuhitimisha kwa tofauti kubwa ambazo zinatofautisha vitu hivi viwili.

1...Rocket huwa inabeba oxygen kwenye vifaa maalumu ili kuisaidia katika swala zima la combustion wakati ndege huwa inategemea Oxygen kutoka katika atmospere.

2... Rocket huwa zinauwezo wa kutoka mpaka nje ya tabaka la dunia kwasababi huwa zinakuwa zimebeba oxygen yake kwenye matangi maalumu ya kuhifadhia oxygen wakati Ndege haziwezi kutoka mpaka nje ya tabaka la dunia kwasababu huko hakuna oxygen na kama tulivyokwisha kufahamu Engine za ndege zinategemea oxygen kutoka kwenye atmosphere ili combustion katika Engine iweze kutokea.
Rocket ikiwa imetoka nje kabisa ya tabaka la dunia
3... Mara nyingi roketi huwa zinaruka zikiwa wima kama unavyoona kwenye picha hapo chini wakati ndege huwa zinaruka kwa ulalo yani ni mpaka ikimbie kwa speed fulani ndipo iweze kuruka.

4... Roketi huwa Zinaviwanja vyake maalumu ambavyo huwa vinatengwa mbali kabisa na makazi ya watu wakati ndege huwa viwanja vyake vinaweza kuwa hata katikati ya miji.
Muonekano wa uwanja wa kurushia roketi
5... Roket inaporuka basi inapomaliza kazi yake ambayo ilikusudiwa kufanya hurudi duniani na kuangukia baharini au hata maeneo ya wazi wakati ndege hurudi chini ardhini na kutumia mataili kutua uwanjani.
Muonekano wa roketi zinapojiachia baada ya kuishiwa nguvu na kurudi duniani kisha kudondokea baharini au maeneo ya wazi... Kinachobaki hapo ni ile iliyokaa kama ndege(space shuttle) tu kisha inendelea na safari baada ya kusindikizwa kwa umbali fulani na rocket
Mwisho

Mpenzi msomaji basi kwa tofauti hizo hapo juu natumaini utakuwa umejifunza mambo kadhaa siku ya leo hivyo usisahau kutembelea page yetu ya facebook kisha tuachie maoni ni jambo gani ungependa tulizungumzie.

Bonyeza hapa kutembelea page yetu ya facebook kisha like ili uweze kupata notification kila tunapotowa post mpya.

Share na wengine.

Comments

Post a Comment

Popular Posts