PAKA WAKUBWA DUNIANI NA SIFA ZAO
Habari ndugu msomaji. Karibu katika makala hii ambayo utaenda kujifunza mambo kadhaa ambayo huenda hukuwahi kuyafahamu kuhusu Paka wakubwa wanaopatikana Duniani huku ukiwa unafahamu aina moja tu ya paka ambao tumezowea kuona wakifugwa majumbani kwetu.
Duniani kuna aina kama 20 hivi za Paka lakini katika aina hizo tutaangalia aina chache tu za paka ambao ni wakubwa na maarufu zaidi tukianza na Paka wa majumbani ( House cats ) kisha kuja kuzungumzia na Paka wa misituni ( wild cats ) Tutajifunza kwa njia ya vionjo yaani Tips.
Paka wa Majumbani ( house cats )
Hii ni aina ya paka ambao wanaishi majumbani na mara huwaga ni tegemezi kwa binadamu kwenye suala la chakula japo huwa nao wanaweza kujitafutia.
Paka huweza kuishi miaka 2 mpaka kufikia miaka 16 huku akifikia uzani wa kilogram 3.6 mpaka 4.5 na kwa kuwa pia kuna aina nyingi ya paka basi kwa ujumla ili uweze kutambua kuwa hii ni aina ya paka wa majumbani basi utaweza kumtambua kwa umbo lake ambalo huwa ni dogo tu na si kubwa sana.
Inaaminika kwamba Paka wa majumbani walianza kufugwa maeneo ya Egypt takribani miaka 9500 iliyopita ( 7500BC ).
Kibailojia sifa ya mnyama huyu hula nyama na huwinda windo lake katika mtindo wa kunyemelea na ana uwezo wa kukimbia mpaka kilometa 48 kwa saa.
Imewahi rekodiwa kwamba Paka kijana mkubwa zaidi aliyevunja rekodi alikuwa na uzani wa kilogram 21 na paka kijana mdogo zaidi duniani alikuwa na uzani wa kilogram 1.
Paka wa Mwituni
Sasa ukiachana na wale paka wa nyumbani zipo aina nyingi sana za paka wanaoishi misituni huku wakiwa na sifa tofauti tofauti na wengine wakiwa ni wakubwa zaidi katika maumbo.
Hebu hapa tuangalie aina hizo za paka na utofauti wao kwa kudodosa baadhi ya sifa zao.
1. Simba ( Lion )
Kati ya wanyama wote wa jamii ya paka, simba ndiyo mrefu (mabegani), na ndio wa pili kwa uzito baada ya tiger. Kwa miguu yake yenye nguvu, taya imara, na meno yake chonge yenye urefu wa sm 8, simba anaweza akamwangusha na kumuua myama mkubwa. Fuvu la kichwa la simba linafanana sana na lile la tiger, hivyo tofauti ya taya zao za chini ndio pekee hutumika kuwatofautisha.
Uzito wa simba wakubwa ni kati ya kg 150 – 250 kwa dume na kg 120 – 182 kwa jike. Simba huwa na ukubwa tofauti kulingana na mazingira na eneo, kusababisha tofauti mbalimbali za rekodi za uzito. Kwa mfano, simba wa kusini mwa Afrika wameonekana kuwa wazito mara tano zaidi ya wale wa Afrika Mashariki, kwa ujumla.
Simba anauwezo wa kukimbia speed ya kilometa 80.5 kwa saa huku akiwa anashika nafasi ya 18 kati ya 19 kwa wanyama wenye speed kali duniani.
Chakula chao ni nyama inayopatikana kwa kuwinda wanyama. Tofauti na paka wengine, simba huishi na kuwinda katika vikundi vyenye wanyama 10-20. Kila kundi lina eneo lake na kuitetea dhidi ya simba wengine. simba jike ndiye anayewinda na baada ya kumkamata mnyama, dume ndiye anayeanza kula na hasa uanza kula viu vya ndani kama vile utumbo, maini, ndipo jike na watoto wanafuata kwa kula.
2. Chui ( leopard )
Chui ni mnyama mwindaji anayewinda kimyakimya saana. Ingawa ni mdogo kuliko wanyama wote wa jenasi ya Panthera, chui bado naweza kuwinda mnyama mkubwa kwasababu ya fuvu lake kubwa lenye taya zenye nguvu. Ukilinganisha na paka wa majumbani mwili wake ni mrefu zaidi na miguu yake ni mirefu.
Urefu wa kichwa na mwili wake ni kati ya ya sm 125 na 165 na mkia ukikaribia sm 60 mpaka 110 huku chui dume ni wa kubwa kwa 30% zaidi ukilinganisha na jike, kufikia uzito wa kg 37 mpaka 91 ukilinganisha na jike wenye kg 28 mpaka 60.
Chui mara nyingi huchanganywa na paka wengine wenye madoa, kama duma na jagwa. Hata hivyo wana mtindo tofauti wa madoa: duma wana madoa ya kawaida yaliyosambaa mwili wote; jaguar wana madoa madogo ndani ya vijimiraba; wakati chui ana madoa ndani ya miduara midogo kuliko ile ya jaguar. Chui ni mkubwa na mwenye misuli zaidi kuliko duma, lakini mdogo kidogo na mwenye misuli kidigo kuliko jaguar. Madoa ya chui ni ya mviringo kwa Afrika Mashiriki na huwa ya mraba kwa kusini mwa Afrika. Chui wameripotiwa kufikia mpaka umri wa miaka 21
Chui anafahamika kwa uwezo wake wa kukwea miti, na huonekana akijipumzisha kwenye matawi ya miti wakati wa mchana, akiburuza mawindo yake mpaka juu ya miti na kuining’iniza huko ingawa, yeye hana nguvu sana kama jamii nyingine ya paka. Chui naye pia ni mwenye nguvu sana, anaweza kukimbia mpaka km 58 kwa saa, kuruka mbele zaidi ya mita 6 na kuruka juu mpaka kufikia hata mita 3.
Chui kiasili ni miongoni mwa wanyama wanaowinda usiku, japo wamerekodiwa mara kadhaa wakiwinda mchana, tena hasa wakati anga likiwa si angavu sana. Wao hutumia muda wao mwingi kulala, aidha juu ya miti, kwenye miamba au kwenye nyasi.
3. Jagwa ( Jaguar )
Imekuwa ni vigumu sana kumtofautisha Jagwa, Chui pamoja na Duma lakini hawa ni paka waliokuwa na tofauti kubwa sana wakilinganishwa. Lakini utaweza kuwafananisha vema kwa kuwatazama mabaka yao tu. Jagwa huwa na mabaka makubwa kiasi na yenye vidoti doti katikati lakini chui akiwa na mabaka madogo yaliyoundwa kwa vidoti tu.
4. Duma ( Cheetah )
Duma naye ni Paka mkubwa wa porini ambaye hula nyama ya wanyama aina ya swala na Hupatikana meneo mengi ya Afrika na eneo kidogo la bara la Asia.
Watu wengi pia hushindwa kumtambua mnyama huyu na badala yake kumuweka katika kundi moja na Chui pamoja na Jagwa.
Utaweza kumtambua duma kwa Kichwa chake kidogo zaidi ukilinganisha na wanyama wengine wa jamii yake kama chui. Duma anatofautiana na chui pia kwa sehemu ya mgongo na sehemu ya machoni: mgongo wa duma huwa kama alama ya "S", tofauti na mgongo wa chui. Macho ya duma yana weusi mkali ukilinganisha na chui.
Tofauti nyingine iliyopo kwa mnyama huyu yeye hutegemea mbio ili kupata windo lake yaani hukimbiza windo lake mpaka kulipata tofauti na hawa wengine wa jamii yake ambao wenyewe hunyemelea mawindo yao.
Duma ndio Paka mwenye kasi zaidi Duniani akiwa anauwezo wa kukimbia kilometa 113 - 120 kwa saa na akiwa ni kiumbe wa 11 kati ya 19 wenye kasi zaidi duniani.
Chui milia wanaishi katika Asia katika pembetatu kati ya Uhindi, Siberia ya kusini na Indonesia. Mazingira wanayoendelea ni misitu. Siku hizi idadi ya chui milia imepungua sana kutokana na upotevu wa maeneo na kuwindwa.
Chakula chao ni nyama inayopatikana kwa kuwinda wanyama. Kama wanyama wengi wanaofanana paka chui milia hupendelea kuvinda pekee yake. Kila mmoja ana eneo lake analoweka alama za kojo na kuitetea dhidi ya chui milia wengine.
Chui milia yeye anauwezo wa kukimbia kilometa 49 - 65 kwa saa huku akiwa na uzani kilogramu 90 - 310 kwa Dume na Jike kilogramu 65 - 170.
Baada ya kuangalia aina hizo hapo juu ya paka wakubwa Duniani na ambao ni maarufu hebu tuangalie na aina nyingine ya paka wakubwa wanaopatikana duniani kwa kutumia Picha.
1. Puma
2. Chui Mawingu
3. Ocelot
4. Serval
5. Caracal
6. Bob cat
Mwisho
Natumanini siku ya leo utakuwa umejifunza jambo juu ya wanyama hawa ambao ni Paka wakubwa hivyo usisahau ku subscribe site yetu katika neno jekundu unaloliona hapo juu ili uwe unapata notification kwenye email yako kila tunapoweka post mpya pia like page yetu ya facebook ( bonyeza hapa kwenda moja kwa moja ) pia usikose makala ijayo itakayoweza kukutambulisha viumbe wenye kasi zaidi waliopo Duniani.
Share na wengine.

Jagwa hufahamika kama Chui wa Amerika Yaani yeye anapatikana sana bara la Amerika ya kusini pamoja na eneo dogo kusini mwa Bara la Amerika ya kaskazini.
Jagwa ana sifa zinazofana sana na chui hiyo niliyezungumzia hapo juu isipokuwa yeye huwa na rangi tofauti ikiwe rangi nyeusi na anauwezo wa kukimbia speed ya kilometa 96.5 kwa saa
4. Duma ( Cheetah )
Duma naye ni Paka mkubwa wa porini ambaye hula nyama ya wanyama aina ya swala na Hupatikana meneo mengi ya Afrika na eneo kidogo la bara la Asia.
Watu wengi pia hushindwa kumtambua mnyama huyu na badala yake kumuweka katika kundi moja na Chui pamoja na Jagwa.
Utaweza kumtambua duma kwa Kichwa chake kidogo zaidi ukilinganisha na wanyama wengine wa jamii yake kama chui. Duma anatofautiana na chui pia kwa sehemu ya mgongo na sehemu ya machoni: mgongo wa duma huwa kama alama ya "S", tofauti na mgongo wa chui. Macho ya duma yana weusi mkali ukilinganisha na chui.
Tofauti nyingine iliyopo kwa mnyama huyu yeye hutegemea mbio ili kupata windo lake yaani hukimbiza windo lake mpaka kulipata tofauti na hawa wengine wa jamii yake ambao wenyewe hunyemelea mawindo yao.
Duma ndio Paka mwenye kasi zaidi Duniani akiwa anauwezo wa kukimbia kilometa 113 - 120 kwa saa na akiwa ni kiumbe wa 11 kati ya 19 wenye kasi zaidi duniani.
5. Chui Milia ( Tiger )
Huyu ni moja ya paka mkubwa saana na ndio mzito zaidi kuliko paka wote. Kwa majina watu wamekuwa wakiumuhusisha na aina nyingine ya paka wakubwa nliokwisha wazungumzia hapo juu lakini huyu ni wa tofauti kabisa na hufahamika zaidi kwa jina la Tiger Chui milia wanaishi katika Asia katika pembetatu kati ya Uhindi, Siberia ya kusini na Indonesia. Mazingira wanayoendelea ni misitu. Siku hizi idadi ya chui milia imepungua sana kutokana na upotevu wa maeneo na kuwindwa.
Chakula chao ni nyama inayopatikana kwa kuwinda wanyama. Kama wanyama wengi wanaofanana paka chui milia hupendelea kuvinda pekee yake. Kila mmoja ana eneo lake analoweka alama za kojo na kuitetea dhidi ya chui milia wengine.
Chui milia yeye anauwezo wa kukimbia kilometa 49 - 65 kwa saa huku akiwa na uzani kilogramu 90 - 310 kwa Dume na Jike kilogramu 65 - 170.
Baada ya kuangalia aina hizo hapo juu ya paka wakubwa Duniani na ambao ni maarufu hebu tuangalie na aina nyingine ya paka wakubwa wanaopatikana duniani kwa kutumia Picha.
1. Puma
2. Chui Mawingu
3. Ocelot
4. Serval
5. Caracal
6. Bob cat
Mwisho
Natumanini siku ya leo utakuwa umejifunza jambo juu ya wanyama hawa ambao ni Paka wakubwa hivyo usisahau ku subscribe site yetu katika neno jekundu unaloliona hapo juu ili uwe unapata notification kwenye email yako kila tunapoweka post mpya pia like page yetu ya facebook ( bonyeza hapa kwenda moja kwa moja ) pia usikose makala ijayo itakayoweza kukutambulisha viumbe wenye kasi zaidi waliopo Duniani.
Share na wengine.
Comments
Post a Comment