Ndege zisizo na madirisha kutoka kampuni ya ndege ya Emirates
Kampuni ya ndege ya Emirates imezindua ndege ambayo imetengezwa na madirisha bandia Badala ya abiria kuweza kuona nje moja kwa moja, sasa watalazimika kutazama picha kutoka nje wakiwa ndani kwa kutumia kamera za fibre-optic.
Emirates inasema kuwa hatua hiyo inatoa fursa ya kuondoa madirisha yote katika ndege za siku zijazo, swala litakalozifanya kuwa nyepesi na kuongeza kasi yake. Rais wa Emirates Sir Tim Clark amesema kuwa picha hizo ni nzuri sana ikilinganishwa na picha zinazotazamwa kwa macho. Madirisha hayo bandia yanapatikana katika chumba cha kwanza cha ndege aina ya Boeing 777-300Er .Sir Tim aliambia BBC lengo lao ni kuwa na ndege isiyo na madirisha kabisa. ''Fikiria ndege isio na madirisha kabisa lakini unapoingia ndani kuna madirisha'', alisema.
Wasi wasi wa kiusalama
Wafanyikazi wa ndege wanatakiwa kuona nje ya ndege iwapo kuna dharura, mtaalam wa usalama wa angani Profesa Graham Braithwaite wa chuo kikuu cha Cranfield University alisema.
"Kuweza kuona nje ya ndege katika dharura ni muhimu, hususan wakati ambapo dharura ya uokoaji inafaa kutekelezwa'', alisema.
"Wahudumu wa ndege watalazimika kuona nje katika dharura , kwa mfano wakati wa moto, kabla ya kufungua mlango na kuanza uokoaji- na kitu chochote ambacho kitahitaji nguvu kufanya hivyo haitakuwa rahisi kuidhinishwa na afisa wa usalama wa angani''. Profesa Braithwaite alisema kwamba kizuizi kikuu katika ndege isiyo na madirisha itakuwa abiria wanavyohisi kuhusu teknolojia hiyo.
'Hakuna mbadala'
Mtaalam wa maswala ya usafiri wa anga John Strickland alisema kuwa ndege zisizo na madirisha zitakuwa na sauti ya chini. hatua hiyo pia itapunguza matumizi ya mafuta iwapo ndege hiyo itakuwa nyepesi. "Chochote kitakachopunguza uzani wa ndege kitapunguza utumizi wa mafuta'', alisema. Hatahivyo, yeye binafsi alipendelea kutaka kuona nje ya ndege : Napenda kuwa na madirisha , kwangu mie madirisha bandia ''sio mbadala''.
Mwisho
Usisahau ku subscribe blogsite yetu ili uwe updated na kila post tutakayoitowa pia pitia facebook u like page yetu ili upate notification kila tunapoweka post mpya. Karibu!.
Comments
Post a Comment