Mapacha walioungana waliowahi kuwa maarufu duniani


Hujambo! Karibu katika makala hii fupi ambayo utaweza kuona ni kwa namna gani baadhi ya mapacha maarufu walio wahi kuishi Duniani huku tukiwa tayari tumewapumzisha ndugu zetu Maria na Consolata Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi Amen.


Mapacha walio ungana wakoje?

Mapacha walioungana huwa ni wachache sana kutokea au kuwepo ,katika watoto laki mbili wanaozaliwa kila mwaka anazaliwa mtoto mmoja tu wa aina hiyo.Watoto wengi huwa hawawezi kuishi ,hufa mara baada ya kuzaliwa au mimba huharibika.Watoto hawa uzaliwa katika uzao wa yai moja,hufanana na wana jinsia moja.
Kuzaliwa kwa watoto hawa huwa kuna hali ya kustaajabisha,kwa ujumla Watoto hao wanaweza kuishi wakizaliwa katika hali hiyo huwa ni kati ya asilimia 5 mpaka asilimia 25 Katika rikodi za historia zinasema kwamba mapacha wa kuungana wengi wanaoweza kuishi kwa muda mrefu ni wa kike,kwa asilimia 70.


Mapacha walioungana wamegawanyika katika sehemu tatu
•73% wameunganika kuanzia kwenye kifua na tumbo
•23% wanakuwa wameunganika katika sehemu ya chini ya mapaja na miguu
•4% wanakuwa wameunganika kichwa


Mapacha walio ungana waliowahi kuwa maarufu Duniani

Eng & Chang
Kwa miaka mingi mapacha walioungana wameendelea kuishi kutokana na matokeo ya tafiti nyingi zilizofanywa na majaribio mengi ya upasuaji yaliyofanyika Mapacha wa kwanza wa kuungana waliojipatia umaarufu mkubwa duniani walijulikana kama 'siamese' majina yao yalikuwa ni Eng na Chang .
Mapacha hao walizaliwa mwaka 1811 waliweza kuishi kwa miaka 63 na kufanikiwa kupata watoto 22 kutoka kwa wadada wawili ndugu waliowaoa wakiwa na umri wa miaka 21,Chang alikuwa na watoto 12 na Eng watoto 10. Walipozaliwa jamii ilitaka kuwauwa lakini kwa kudhaniwa kuwa wataleta mikosi na walioneka kuwa nio viumbe wa ajabu.


Mapacha wa kuungana na maisha yao ya ndoa

Katika karne ya ishirini,mapacha wa kuungana walikuwa wanazuiwa kuoa au kuolewa nchini Marekani Na hii iliibua hisia za wengi pale ambapo wanamuziki ambao ni wacheza filamu wa nchi hiyo Daisy na Violet walipotaka kuolewa.
Watu wengi waliwaona kuwa maumbile yao hayawezi kuwaruhusu kuolewa au kupata wenza ingawa mapacha wenyewe wanajiona wamekamilika.
Kwa upande wa Chang na Eng ambao walifanikiwa kuoa, maisha yao ya ndoa yalikuwa na changamoto nyingi hasa pale ambapo wake zao walipoanza kugombana na kupelekea wake hao kuishi kwenye nyumba mbili tofauti.
Kwa maisha yao yote mapacha hao walikuwa wanaishi kwa mke mmoja siku tatu na mwingine siku tatu. Vilevile mapacha kutoka Tanzania,Consolata na Maria ndoto yao kubwa baada ya shule ilikuwa ni kuolewa na mume mmoja.

Mwisho
Usisahau ku subscribe blogsite yetu ili upate notification kwa email kila tunapoweka post mpya na pia like page yetu ya facebook ili upate notification na usome post kwa wakati kila inapotolewa. Karibu.

Comments

Popular Posts