LIFAHAMU DARAJA LA AINA YAKE CHINA


Kutana Daraja hili la aina yake Duniani likifahamika kwa jina la Zhangjiajie Glass Bridge ambalo lilifunguliwa mnamo August 20, 2016 nchini China. Daraja hili limejipatia umaarufu mkubwa sana Duniani kutokana na kutengenezwa kwa kioo chenye teknolojia maalumu.

Daraja hili limejengwa kwaajili ya kuwavutia watalii likiwa na kioo ambacho ni Transparent hivyo unapokuwa unapita kwenye daraja hili huoni kitu unapokanyaga mithili ya mtu anae elea hewani Tazama video hapa chini.



Kitu cha kuvutia zaidi kilicho litambulisha zaidi daraja hili ni kutokana na kujengwa kwa teknolojia maalumu ambapo wakati unatembea linaweza likakuletea dhihaka kama linataka kupasuka vile kwa nyufa nyufa zitazokuwa zinajitokea. ( bonyeza hapa uone video ya vituko vinavyotokea kwenye daraja hilo)
Muonekano wa aina ya kioo kilicho tumika kwenye daraja hilo hakionekani vizuri ni kama mtu unaelea hewani
Daraja hilo limejengwa likiwa na urefu wa mita 430, upana wa mita 6 na mita 360 kutoka ardhini ambapo ni sawa na urefu wa viwanja vitatu na nusu vya mpira wa miguu. Wakati linafunguliwa hili ndio lilikuwa daraja refu zaidi Duniani la Glass.
Muonekano wa daraja hilo kutoka juu
Daraja hili limejengwa katika kati ya miamba mikubwa miwili ya mlima unaopataikana katika Zhangjiajie National Forest Park. Pia daraja hilo linauwezo wa kubeba watu 800 kwa wakati mmoja huku mtengenezaji aliye design daraja hilo akiwa ni Raia kutoka Israel akifaamika kwa jina la Haim Dotan.

Kutokana na Uwingi wa watalii wanaokwenda kutalii katika daraja hilo basi kwa siku daraja hilo hutembelewa na watu wapatao 8,000.
Msongamano wa watu wakiwa wanatalii katika daraja hilo.
Basi kwa makala hii fupi natumaini utakuwa umejifunza kitu siku ya leo hivyo waweza tembelea youtube channel yetu na ku subscribe ili upate notification kila tunapotowa video mpya pia tembelea facebook page yetu kisha Like ili uwe updated na kila post tutakayoitowa. Hakika utajifunza mengi sana yanakuja.

Bonyeza hapa kwenda moja kwa moja kwenye youtube channel yetu

Pia bonyeza hapa kwenda kwenye page yetu ya facebook moja kwa moja.

Karibu sana.

Comments

Popular Posts