Skip to main content
JINSI YA KUFUFUA FLASH ZILIZOKUFA
Najuwa raia wengi
sana mmejaza flash ambazo ni mbovu majumbani kwenu au kama sio hvyo
mmeshatupa flash nyingi sana kisa zimeharibika pasipo kujuwa flash yako
unaweza ukairudisha na ikawa kama ilivyokuwa. Basi kama una flash
zilizoharibika kuna njia #Tatu za kuirudisha flash yako kwahyo kuwa makini na hizi njia hapo na chini na uangalie ipi itakuwa ni rahisi kwako..
Kila kifaa kinachochomekwa kwenye kompyuta basi huonekana kwa jina au
herufi kwa mbele basi kwa kubadilisha jina na herufi ya flash yako
unaweza kufanya flash yako kufanya kazi tena kama ilivyokuwa pale awali (
kumbuka njia hii ni kwa wale ambao flash yao inaonekana lakini haiwezi
kufunguka )
¤ jinsi ya kubadili jina
Kabla ya yote hakikisha umechomeka flash yako kwenye kompyuta. Baada ya hapo nenda kwenye icon ya #my_computer au wengine imeandikwa #This_pc kisha bonyeza batani ya kulia kwenye mouse yako kisha bonyeza neno #manage... Baada ya hapo chagua neno #disk_management
iliyoko upande wa kushoto chini kidogo... Kisha chagua Flash au memory
unayotaka kurekebisha au kuifufua kisha bofya batani ya kulia ya mouse
yako kisha chagua #change_drive_letters_and_path.
Baada ya hapo chagua herufi kwenye list inayoonekana upande wa kulia(
hakikisha unachagua herufi ambayo haitumiki au haijatumika kabisa kwenye
kompyuta yako) baada ya hapo bonyeza #ok kisha hapo hapo utaona flash yako imerudi na kuwa kama mwanzo.
Kuna wakati flash inashindwa kuonekana kwenye kompyuta yako kwasababu
kompyuta yako inashindwa kugundua driver za flash yako. Hivyo kwa
kutumia njia hii utaweza kuondoa driver zilizopo kwenye kompyuta yako na
kuzirudisha tena ili kiwezesha kompyuta yako kugundua driver hizo ili
flash yako iweze kuonekana.
¤ Jinsi ya ku install driver
Chomeka flash yako kisha nenda kwenye icon ilioandikwa #My_computer au
#This_pc kisha bofya kibonyezeo cha kulia kwenye mouse yako kisha chagua
neno #manage baada ya hapo chagua #device_manager iliyoko upande wa kushoto chini kidogo. Baada ya hapo chagua #disk_drives iliyoko juu kabisa na utachagua jina la flash yako kisha kisha libonyeze jina hilo alafu utabonyeza #uninstall kisha utabonyeza #ok.
Baada ya happ chomoa flash yako kisha #restart
kompyuta yako na ikishawaka tena chomeka flash yako alafu iache kwa
muda kama hata dakika moja au hata dakika mbili ili iweze ku install
driver zote kisha baada ya kumaliza yenyewe utaona flash yako
inajifungua yenyewe
Njia hii ni moja kati ya njia ambazo zinahitaji umakini mkubwa sana
kwasababu ni njia ambayo inachanganya kidogo lakini njia hii ndio
imeonekana ikisaidia wengi zaidi
¤ Hatua
Chomeka flash
yako kwenye kompyuta na hakikisha hakuna kifaa kingne chochote kilicho
chomekwa kwenye kompyuta yako zaidi ya flash hiyo. Fungua program ya #CMD au program ya #COMMAND_PROMPT kwenye kompyuta yako... Baada ya hapo andika #diskpart kisha bonyeza #enter kama itauliza ruhusa basi bonyeza #ok kisha endelea na hatua zinazofuata.
Kisha tena andika #List_disk
kisha bofya #enter na hapo utaweza kuona vifaa vyako vyote
ulivyovichomeka kwenye kompyuta ikiwema flash au hard disk ambayo
unataka kuifufua... Baada ya hapo kwa umakini angalia namba ya disk
ambayo unataka kuifufua kisha andika #select_disk kisha andika namba ya disk kwa mbele ya maneno kisha bofya #Enter.
Baada ya hapo andika #Clean kisha bofya #Enter na kisha andika #create_partition_primary
na baada ya hapo andika #active na bofya #Enter. Baada ya hapo andika
#select_partition_1 kisha bofya #Enter na baada ya hapo andika
#format_fs=fat32 kisha bofya #Enter.
Baada ya kufata hatua zote
hapo juu kwa umakini subiri kwa muda kidogo na pale itakapomaliza ku
format flash yako basi itakuwa tayari kwa kutumia na hakika itakuwa
imefufuka kabisa.
#mwisho
( kabla hujafanya kwa kusoma
lazma itakuchanganya sana lakini wakati wa kufanya utaona simple kwa
kufatilia post hii kwa umakini.)
Tunaomba u like page yetu kisha share page yetu ili isambae zaidi na sisi tutazidi kuleta post makini zaidi.
Share post hii mara nyingi uwezavyo.
#TWoTT
Mambo ,nahitaji kupata maujanja zaidi ,mnanisaidiaje ili niwe karibu na nyie
ReplyDelete