TOFAUTI KATI YA BATTERY ZA LI-ION NA LI-PO
Tumezungumzia vitu mbali mbali kwenye simu lakini bado kuna vitu vingi sana bado tunahitaji kuvielewa kwahivyo leo nimeona tuangalie tofauti kati ya hizo battery za aina mbili ambazo ni battery za Li-ion pamoja na Li-po kama tujuavyo kuna simu zinakuja zikiwa na battery aina tofauti mfano utakuta kwenye baadhi ya simu utakuta zina battery limeandikwa Li-ion 2500mAh au nyingne utakuta zimeandikwa Li-po 2500mAh. Sasa hebu tutofautishe battery hizi na mwishoni uje ugundue mwenyewe battery ipi ni bora zaidi.
battery za Li-ion
Muonekano wa battery za Li-ion |
Kingine kitu cha tofauti kwenye battery za Li-ion huwa zinaharibika kutokana na umri au muda yaani muda unavyozidi kwenda basi na battery yenyewe ndivyo inavyokaribia umri wake wa kufa au kuharibika yani kwa kifupi haziwezi kuishi muda mrefu zikiwa na uwezo wake ule ule.
Sifa za battery za Li-ion
> Hali ya hewa... Battery hizi zinauwezo mzuri wa kufanya kazi kwenye hali ya hewa ya 4° F mpaka 140° F (-20° C to 60° C)
> Matumizi... Mara nyingi battery hizi hutumika kwenye vifaa kama simu za mkononi, digital camera pamoja na kompyuta za mkononi( laptop).
> Maisha ya battery... Battery hizi huwa zinapoteza 0.1% kila mwezi
> Muundo... Kutokana na kemikali zinazotumika kutengenezea battery hizi basi battery hizi huwezekana kuwa na muundo wa mstatili tu.
> Usalama... Kutokana na kemikali zilizotumika kutenezea aina hii ya battery basi likikaa kwenye joto lililozidi au zikivuja basi uwezekano wa kuripuka huwa ni rahisi sana.
Battery za Li-po
Muonekana wa battery za Li-po |
Aina hii ya battery huwa na uwezo wa kutengenezwa zikiwa nyembamba sana tofauti na battery za Li-ion... Battery hizi zina gharama kutengeneza na zinaweza kutengenezwa zikiwa nyepesi sana lakini zikawa na uwezo ule ule wa kuhifadhi chaji.
Tatizo la battery hizi huwa hazina uwezo wa kutunza chaji kwa muda mrefu kama zilivyo battery za Li-ion lakini pamoja na kwamba battery hizi hazina uwezo wa kutunza chaji kwa muda mrefu pia battery hizi huwa zina maisha mafupi sana kuliko zile battery za Li-ion.
Sifa za battery za Li-po
> Hali ya hewa... Battery hizi zinauwezo mkubwa wa kufanya kazi kwenye joto kali zaidi au hata kwenye baridi kali.
> Matumizi... Pia battery hizi hutumika kwenye vifaa kama simu za mkononi, camera na hata kompyuta za mkononi.
> Maisha ya battery... Battery hizi za Li-po hazina maisha marefu kama battery za Li-ion
> Muundo... Kutokana na kemikali zilizotumika kutengenezea battery Za Li-po basi huweza kuwa na muundo wowote kutokana na kifaa chenyewe kilivyo na pia battery hizi huwa nyembamba tofauti na za Li-ion.
> Usalama... Kutokana na hali ya hewa battery hizi mara nyingi huwa ni vigumu kulipuka (ingawa zinaweza kulipuka kutokana na kisababishi) na pia huwa na uwezekano mdogo sana wa kuvuja.
Mwisho
Basi kutokana na ufafanuzi huo hapo pamoja na kuangalia tofauti na sifa za aina hizo za battery tunaona kwamba battery za Li-ion ni battery bora zaidi kuliko battery za Li-po hivyo basi ni vema unapoenda kununua simu ukachunguza kwanza simu hiyo unayokwenda kununua ina safi gani kwa upande wa battery kama tulivyokwisha zungumzia battery hizo kwenye makala hii.
Tembelea page yetu ya Facebook kisha tuachie maoni yako au mapendekezo yako ni jambo gani ambalo ungependa tulizungumzie kisha Like page yetu ili usipitwe na Post yoyote tutakayotoa.
Bonyeza hapa kutembelea Page yetu ya facebook moja kwa moja. Karibu sana.
Share na wangine.
Comments
Post a Comment